Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 111

Sifa Za Bwana Kwa Matendo Ya Ajabu

1 Msifuni Bwana.

Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote,

katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.

2 Kazi za Bwana ni kuu,

wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.

3 Kazi zake zimejaa fahari na utukufu,

haki yake hudumu daima.

4 Amefanya maajabu yake yakumbukwe,

Bwana ni mwenye neema na huruma.

5 Huwapa chakula wale wanaomcha,

hulikumbuka agano lake milele.

6 Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake,

akiwapa nchi za mataifa mengine.

7 Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki,

mausia yake yote ni ya kuaminika.

8 Zinadumu milele na milele,

zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.

9 Aliwapa watu wake ukombozi,

aliamuru agano lake milele:

jina lake ni takatifu na la kuogopwa.

10 Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,

wote wanaozifuata amri zake wana busara.

Sifa zake zadumu milele.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também