Publicidade

Salmos 24

Mfalme Mkuu
Zaburi ya Daudi.

1 Dunia ni mali ya Bwana, na vyote vilivyomo ndani yake,

ulimwengu, na wote waishio ndani yake,

2 maana aliiwekea misingi yake baharini

na kuifanya imara juu ya maji.

3 Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana?

Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?

4 Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe,

yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake

au kuapa kwa kitu cha uongo.

5 Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana,

na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.

6 Hiki ndicho kizazi cha wale wamtafutao,

wale wautafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

7 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,

inukeni enyi milango ya kale,

ili mfalme wa utukufu apate kuingia.

8 Ni nani huyu Mfalme wa utukufu?

Ni Bwana aliye na nguvu na uweza,

ni Bwana aliye hodari katika vita.

9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,

viinueni juu enyi milango ya kale,

ili Mfalme wa utukufu apate kuingia.

10 Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu?

Ni Bwana Mwenye Nguvu Zote;

yeye ndiye Mfalme wa utukufu.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-