Publicidade

Salmos 110

Bwana Na Mfalme Wake Mteule
Zaburi ya Daudi.

1 Bwana amwambia Bwana wangu:

"Keti mkono wangu wa kuume,

mpaka nitakapowafanya adui zako

kuwa mahali pa kuweka miguu yako."

2 Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;

utatawala katikati ya adui zako.

3 Askari wako watajitolea kwa hiari

katika siku yako ya vita.

Ukiwa umevikwa fahari takatifu,

kutoka tumbo la mapambazuko

utapokea umande wa ujana wako.

4 Bwana ameapa,

naye hatabadilisha mawazo yake:

"Wewe ni kuhani milele,

kwa mfano wa Melkizedeki."

5 Bwana yuko mkono wako wa kuume,

atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.

6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga

na kuwaponda watawala wa dunia nzima.

7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia,

kwa hiyo atainua kichwa chake juu.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-