Publicidade

Salmos 75

Mungu Ni Mwamuzi
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa "Usiharibu!" Zaburi ya Asafu. Wimbo.

1 Ee Mungu, tunakushukuru,

tunakushukuru wewe,

kwa kuwa jina lako li karibu;

watu husimulia matendo yako ya ajabu.

2 Unasema, "Ninachagua wakati maalum;

ni mimi nihukumuye kwa haki.

3 Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka,

ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.

4 Kwa wale wenye majivuno ninasema,

‘Msijisifu tena,’

kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.

5 Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu;

msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ "

6 Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi

au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.

7 Bali Mungu ndiye ahukumuye:

Humshusha huyu na kumkweza mwingine.

8 Mkononi mwa Bwana kuna kikombe

kilichojaa mvinyo unaotoka povu

uliochanganywa na vikolezo;

huumimina, nao waovu wote wa dunia

hunywa mpaka tone la mwisho.

9 Bali mimi, nitatangaza hili milele;

nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.

10 Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote,

bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-