Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 6

Sala Kwa Ajili Ya Msaada Wakati Wa Taabu

Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi.6:0 Sheminithi ni mtajo mmojawapo katika lugha ya uimbaji. Zaburi ya Daudi.

1 Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako,

wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.

2 Unirehemu Bwana,

kwa maana nimedhoofika;

Ee Bwana, uniponye,

kwa maana mifupa yangu

ina maumivu makali.

3 Nafsi yangu ina uchungu mwingi.

Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini?

4 Geuka Ee Bwana, unikomboe,

uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.

5 Hakuna mtu anayekukumbuka

akiwa amekufa.

Ni nani awezaye kukusifu

akiwa kuzimu?

6 Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;

usiku kucha nafurikisha

kitanda changu kwa machozi;

nimelowesha viti vyangu vya fahari

kwa machozi.

7 Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,

yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.

8 Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,

kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu.

9 Bwana amesikia kilio changu kwa huruma,

Bwana amekubali sala yangu.

10 Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,

watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também