Publicidade

Salmos 114

Maajabu Ya Mungu Wakati Israeli Walipotoka Misri

1 Wakati Israeli walipotoka Misri,

nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni,

2 Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu,

Israeli akawa milki yake.

3 Bahari ilitazama ikakimbia,

Yordani ulirudi nyuma,

4 milima ilirukaruka kama kondoo dume,

vilima kama wana-kondoo.

5 Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia,

nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma,

6 enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume,

enyi vilima, kama wana-kondoo?

7 Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana,

mbele za Mungu wa Yakobo,

8 aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji,

mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-