Publicidade

Salmos 100

Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu
Zaburi ya shukrani.

1 Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.

2 Mwabuduni Bwana kwa furaha;

njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.

3 Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu.

Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;

sisi tu watu wake,

kondoo wa malisho yake.

4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani

na katika nyua zake kwa kusifu,

mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.

5 Kwa maana Bwana ni mwema

na upendo wake wadumu milele;

uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-