Publicidade

Salmos 16

Sala Ya Matumaini
Utenzi wa Daudi.

1 Ee Mungu, uniweke salama,

kwa maana kwako nimekimbilia.

2 Nilimwambia Bwana, "Wewe ndiwe Bwana wangu;

pasipo wewe sina jambo jema."

3 Kwa habari ya watakatifu walioko duniani,

ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.

4 Huzuni itaongezeka kwa wale

wanaokimbilia miungu mingine.

Sitazimimina sadaka zao za damu

au kutaja majina yao midomoni mwangu.

5 Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu;

umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.

6 Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri,

hakika nimepata urithi mzuri.

7 Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri,

hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.

8 Nimemweka Bwana mbele yangu daima.

Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,

sitatikisika.

9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia;

mwili wangu nao utapumzika salama,

10 kwa maana hutaniacha kaburini,

wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu.

11 Umenijulisha njia ya uzima;

utanijaza na furaha mbele zako,

pamoja na furaha za milele

katika mkono wako wa kuume.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-