Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 130

Kuomba Msaada

Wimbo wa kwenda juu.

1 Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.

2 Ee Bwana, sikia sauti yangu.

Masikio yako na yawe masikivu

kwa kilio changu unihurumie.

3 Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi,

Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?

4 Lakini kwako kuna msamaha,

kwa hiyo wewe unaogopwa.

5 Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,

katika neno lake naweka tumaini langu.

6 Nafsi yangu inamngojea Bwana

kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,

naam, kuliko walinzi

waingojeavyo asubuhi.

7 Ee Israeli, mtumaini Bwana,

maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma,

na kwake kuna ukombozi kamili.

8 Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli

kutoka dhambi zao zote.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também