Publicidade

Salmos 141

Maombi Ya Kuhifadhiwa Dhidi Ya Uovu
Zaburi ya Daudi.

1 Ee Bwana, ninakuita wewe, uje kwangu hima.

Sikia sauti yangu ninapokuita.

2 Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba;

kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni.

3 Ee Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu,

weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.

4 Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya,

nisije nikashiriki katika matendo maovu

pamoja na watu watendao mabaya,

wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa.

5 Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma;

na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu.

Kichwa changu hakitalikataa.

Hata hivyo, maombi yangu daima

ni kinyume cha watenda mabaya,

6 watawala wao watatupwa chini

kutoka kwenye majabali,

waovu watajifunza kwamba maneno yangu

yalikuwa kweli.

7 Watasema, "Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi,

ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi."

8 Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mwenyezi,

ndani yako nimekimbilia, usiniache nife.

9 Niepushe na mitego waliyonitegea,

kutokana na mitego iliyotegwa na watenda mabaya.

10 Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe,

wakati mimi ninapita salama.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-