Publicidade

Salmos 126

Kurejezwa Kutoka Utumwani
Wimbo wa kwenda juu.

1 Bwana alipowarejeza mateka Sayuni,

tulikuwa kama watu walioota ndoto.

2 Vinywa vyetu vilijaa kicheko,

ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.

Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,

"Bwana amewatendea mambo makuu."

3 Bwana ametutendea mambo makuu,

nasi tumejaa furaha.

4 Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa,

kama vijito katika Negebu.

5 Wapandao kwa machozi

watavuna kwa nyimbo za shangwe.

6 Yeye azichukuaye mbegu zake

kwenda kupanda, huku akilia,

atarudi kwa nyimbo za shangwe,

akichukua miganda ya mavuno yake.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-