Publicidade

Salmos 11

Kumtumaini Bwana
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 Kwa Bwana ninakimbilia,

unawezaje basi kuniambia:

"Ruka kama ndege kwenye mlima wako.

2 Hebu tazama, waovu wanapinda pinde zao,

huweka mishale kwenye uzi wake,

wakiwa gizani ili kuwapiga

wale wanyofu wa moyo.

3 Wakati misingi imeharibiwa,

mwenye haki anaweza kufanya nini?"

4 Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu;

Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.

Huwaangalia wana wa watu,

macho yake yanawajaribu.

5 Bwana huwajaribu wenye haki,

lakini waovu na wanaopenda jeuri,

nafsi yake huwachukia.

6 Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali

na kiberiti kinachowaka,

upepo wenye joto kali ndio fungu lao.

7 Kwa kuwa Bwana ni mwenye haki,

yeye hupenda haki.

Wanyofu watauona uso wake.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-