Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 138

Maombi Ya Shukrani

Zaburi ya Daudi.

1 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, kwa moyo wangu wote,

mbele ya "miungu" nitaimba sifa zako.

2 Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu,

nami nitalisifu jina lako

kwa ajili ya upendo wako

na uaminifu,

kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako

juu ya vitu vyote.

3 Nilipoita, ulinijibu;

ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari.

4 Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Bwana,

wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako.

5 Wao na waimbe kuhusu njia za Bwana,

kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.

6 Ingawa Bwana yuko juu,

humwangalia mnyonge,

bali mwenye kiburi

yeye anamjua kutokea mbali.

7 Nijapopita katikati ya shida,

wewe unayahifadhi maisha yangu,

unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu,

kwa mkono wako wa kuume unaniokoa.

8 Bwana atatimiza kusudi lake kwangu,

Ee Bwana, upendo wako wadumu milele:

usiziache kazi za mikono yako.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também