Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 87

Sifa Za Yerusalemu

Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.

1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni

kuliko makao yote ya Yakobo.

3 Mambo matukufu yanasemwa juu yako,

ee mji wa Mungu:

4 "Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu87:4 Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri. na Babeli

miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:

Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,87:4 Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.

nami nitasema, Huyu alizaliwa Sayuni.’ "

5 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,

"Huyu na yule walizaliwa humo,

naye Aliye Juu Sana mwenyewe

atamwimarisha."

6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa:

"Huyu alizaliwa Sayuni."

7 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,

"Chemchemi zangu zote ziko kwako."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também