Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 52

Hukumu Ya Mungu

Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi. Baada ya Doegi, Mwedomu kumwendea Sauli na kumjulisha kuwa: "Daudi amekwenda nyumbani kwa Ahimeleki."

1 Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya?

Kwa nini unajivuna mchana kutwa,

wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu?

2 Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi.

Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila.

3 Unapenda mabaya kuliko mema,

uongo kuliko kusema kweli.

4 Unapenda kila neno lenye kudhuru,

ewe ulimi wenye hila!

5 Hakika Mungu atakushusha chini

kwa maangamizi ya milele:

atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu

kutoka hema yako,

atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai.

6 Wenye haki wataona na kuogopa,

watamcheka, wakisema,

7 "Huyu ni yule mtu ambaye

hakumfanya Mungu kuwa ngome yake,

bali alitumainia wingi wa utajiri wake,

na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!"

Neema Ya Mungu

8 Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni

unaostawi katika nyumba ya Mungu,

nautegemea upendo wa Mungu usiokoma

milele na milele.

9 Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda,

nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema.

Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também