Publicidade

Salmos 12

Kuomba Msaada
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi.

1 Bwana tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka;

waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.

2 Kila mmoja humwambia jirani yake uongo;

midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.

3 Bwana na akatilie mbali midomo yote ya hila

na kila ulimi uliojaa majivuno,

4 ule unaosema, "Kwa ndimi zetu tutashinda;

midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?"

5 "Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge

na kulia kwa uchungu kwa wahitaji,

nitainuka sasa," asema Bwana.

"Nitawalinda kutokana na wale

wenye nia mbaya juu yao."

6 Maneno ya Bwana ni safi,

kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,

iliyosafishwa mara saba.

7 Ee Bwana, utatuweka salama

na kutulinda na kizazi hiki milele.

8 Watu waovu huenda wakiringa kila mahali

wakati ambapo yule aliye mbaya sana

ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-