Publicidade

Salmos 13

Sala Ya Kuomba Msaada
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 Mpaka lini, Ee Bwana? Je, utanisahau milele?

Utanificha uso wako mpaka lini?

2 Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini,

na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu?

Adui zangu watanishinda mpaka lini?

3 Nitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu.

Yatie nuru macho yangu,

ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.

4 Adui yangu atasema, "Nimemshinda,"

nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

5 Lakini ninategemea upendo wako usiokoma;

moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.

6 Nitamwimbia Bwana,

kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-