Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 9:20-22

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

20 Wakati huo huo, mwanamke mmoja, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu, akagusa upindo wa vazi lake, 21 kwa maana alisema moyoni mwake, "Kama nikigusa tu vazi lake, nitaponywa."

22 Yesu akageuka, naye alipomwona akamwambia, "Binti, jipe moyo mkuu, imani yako imekuponya." Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa ile ile.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    20 Wakati huo huo, mwanamke mmoja, aliyekuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na mbili, akaja nyuma ya Isa, akagusa upindo wa vazi lake, 21 kwa maana alisema moyoni mwake, "Nikigusa tu vazi lake, nitaponywa."

    22 Isa akageuka, naye alipomwona akamwambia, "Binti, jipe moyo, imani yako imekuponya." Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa hiyo.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    20 Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake. 21 Mt 14:36Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. 22 Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.