Kukamilika Kwa Ukuta
15 Basi ukuta ukakamilika siku ya ishirini na tano mwezi wa Eluli,6:15 Eluli ni mwezi wa sita kwenye kalenda ya Kiyunani; katika kalenda yetu ni Agosti/Septemba. kazi ambayo ilichukua siku hamsini na mbili. 16 Adui zetu wote waliposikia kuhusu hili, mataifa yote yaliyotuzunguka yakaogopa na kupoteza ujasiri, kwa sababu yalitambua kuwa kazi hii imefanyika kwa msaada wa Mungu wetu.