Pular para o conteúdo
Publicidade

Hesabu 13:31-33

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, "Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kutuliko sisi." 32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, "Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu. 33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, "Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kuliko sisi." 32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, "Nchi tuliyoipeleleza hula watu wanaoishi ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu. 33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili). Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    31 Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. 32 Mt 23:13;Amo 2:9Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala wakazi wake; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu wakubwa mno. 33 Mwa 6:4;1 Sam 17:4-7;Isa 40:22Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.