31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, "Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kuliko sisi." 32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, "Nchi tuliyoipeleleza hula watu wanaoishi ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu. 33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili). Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona."