Watu Wanaasi
1 Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu. 2 Waisraeli wote wakanungʼunika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, "Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa! 3 Kwa nini Bwana anatuleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watachukuliwa kama nyara. Je, isingekuwa bora kwetu kurudi Misri?" 4 Wakasemezana wao kwa wao, "Inatupasa kumchagua kiongozi na kurudi Misri."