Pular para o conteúdo
Publicidade

Hesabu 14:1-4

SRUV Swahili Revised Union Version

Watu wanaasi

1 Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule. 2 Zab 106:25;Kum 28:68Kisha wana wa Israeli wote wakamnung’unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. 3 Mbona BWANA anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri? 4 Neh 9:17;Mdo 7:39;Ebr 11:15Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe kiongozi, tukarudi Misri.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu. 2 Waisraeli wote wakanung’unika dhidi ya Musa na Haruni, na kusanyiko lote wakawaambia, "Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa! 3 Kwa nini Mwenyezi Mungu anatuleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watachukuliwa kama nyara. Je, isingekuwa bora kwetu kurudi Misri?" 4 Wakasemezana wao kwa wao, "Inatupasa kumchagua kiongozi na kurudi Misri."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu. 2 Waisraeli wote wakanungʼunika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, "Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa! 3 Kwa nini Bwana anatuleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watachukuliwa kama nyara. Je, isingekuwa bora kwetu kurudi Misri?" 4 Wakasemezana wao kwa wao, "Inatupasa kumchagua kiongozi na kurudi Misri."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.