Pular para o conteúdo
Publicidade

Hesabu 2

Amri ya kupiga kambi na kuingia

1 BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2 Hes 1:52;24:2-9 Wana wa Israeli watapanga kila mtu penye bendera yake mwenyewe, na alama za nyumba za baba zao; kuikabili hema ya kukutania ndiko watakakopanga kwa kuizunguka pande zote. 3 Hes 10:14;Rut 4:20;1 Nya 2:10;Mt 1:4;Lk 3:32,33 Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea maawio ya jua, ndio wale wa bendera ya kambi ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu. 4 Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sabini na nne na mia sita. 5 Hes 7:18,23 Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila la Isakari; na mkuu wa wana wa Isakari atakuwa Nethaneli mwana wa Suari; 6 Hes 26:25 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu hamsini na nne na mia nne; 7 Mwa 49:13;Kum 33:18 na kabila la Zabuloni; na mkuu wa wana wa Zabuloni atakuwa Eliabu mwana wa Heloni; 8 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu hamsini na saba na mia nne. 9 Hes 10:14;1 Nya 5:2;Zab 78:52 Hao wote waliohesabiwa katika kambi ya Yuda walikuwa elfu mia moja themanini na sita na mia nne, kwa makundi yao. Hao ndio watakaotangulia mbele.

10 Kum 33:6;1 Nya 5:1 Upande wa kusini kutakuwa na bendera ya kambi ya Reubeni kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Reubeni atakuwa Elisuri mwana wa Shedeuri. 11 Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu arubaini na sita na mia tano. 12 Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila la Simeoni; na mkuu wa wana wa Simeoni atakuwa Shelumieli mwana wa Suri-shadai; 13 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu hamsini na tisa na mia tatu; 14 na kabila la Gadi; na mkuu wa wana wa Gadi atakuwa Eliasafu mwana wa Deueli; 15 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu arubaini na tano, mia sita na hamsini. 16 Hes 10:18;Mwa 49:3;1 Nya 5:1 Wote waliohesabiwa katika kambi za Reubeni walikuwa elfu mia moja hamsini na moja na mia nne na hamsini, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaofuata wakiwa kundi la pili.

17 Mdo 7:44;Ebr 8:2;1 Kor 14:40 Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na kambi za Walawi katikati ya kambi zote; kama wapangavyo kambi, watasafiri vivyo hivyo, kila mtu mahali pake, penye bendera zao.

18 Mwa 48:14-20;Zab 80:1;Hos 11:3 Upande wa magharibi kutakuwa na bendera ya kambi ya Efraimu kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Efraimu atakuwa Elishama mwana wa Amihudi. 19 Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na mia tano. 20 Na karibu naye itakuwa kabila la Manase; na mkuu wa wana wa Manase atakuwa Gamalieli mwana wa Pedasuri; 21 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu thelathini na mbili na mia mbili; 22 Zab 68:27;Ufu 7:8 tena kabila la Benyamini; na mkuu wa wana wa Benyamini atakuwa Abidani mwana wa Gideoni; 23 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu thelathini na tano na mia nne. 24 Hes 10:22 Wote waliohesabiwa katika kambi ya Efraimu walikuwa elfu mia moja na nane na mia moja, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaoondoka wakiwa kundi la tatu.

25 Kum 32:22 Upande wa kaskazini kutakuwa na bendera ya kambi ya Dani kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Dani atakuwa Ahiezeri mwana wa Amishadai. 26 Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sitini na mbili na mia saba. 27 Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila la Asheri; na mkuu wa wana wa Asheri atakuwa Pagieli mwana wa Okrani; 28 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu arubaini na moja na mia tano; 29 Mwa 30:8;49:21;2 Fal 15:29;Ufu 7:6 kisha kabila la Naftali; na mkuu wa wana wa Naftali atakuwa Ahira mwana wa Enani; 30 na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu hamsini na tatu na mia nne. 31 Hes 10:25 Wote waliohesabiwa katika kambi ya Dani walikuwa elfu mia moja hamsini na saba na mia sita. Hao ndio watakaoondoka mwisho kwa kufuata bendera2:31 Katika Kiebrania ni ‘kufuata vikosi vyao’. yao.

32 Kut 12:37;38:26;Hes 1:46;11:21 Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli kwa nyumba za baba zao; wote waliohesabiwa katika kambi kwa majeshi yao, walikuwa elfu mia sita na tatu na mia tano na hamsini. 33 Hes 1:47;26:57-62 Lakini Walawi hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli; kama BWANA alivyomwagiza Musa. 34 Kut 39:42;Hes 24:2,9;Zab 119:6;Isa 45:12;Lk 1:6;1 Kor 14:40 Hivyo ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama BWANA alivyomwamuru Musa; ndivyo walivyojipanga kufuata bendera zao, na ndivyo walivyosafiri, kila mtu kwa jamaa zao, kwa nyumba za baba zao.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também