Pular para o conteúdo
Publicidade

Hesabu 6:2,3,5,6

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

2 "Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Ikiwa mwanaume au mwanamke anataka kuweka nadhiri maalum, nadhiri ya kutengwa kwa ajili ya Bwana kama Mnadhiri, 3 ni lazima ajitenge na mvinyo na kinywaji kingine chochote chenye chachu, na kamwe asinywe siki itokanayo na mvinyo au itokanayo na kinywaji kingine chenye chachu. Kamwe asinywe maji ya zabibu wala kula zabibu mbichi au kavu.

5 " ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya Bwana, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu mpaka kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya Bwana kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke. 6 Kwa kipindi chochote cha kujitenga kwa ajili ya Bwana hatakaribia maiti.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    2 "Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Ikiwa mwanaume au mwanamke anataka kuweka nadhiri maalum, nadhiri ya kutengwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama Mnadhiri, 3 ni lazima ajitenge na mvinyo na kinywaji kingine chochote chenye chachu, na kamwe asinywe siki itokanayo na mvinyo au itokanayo na kinywaji kingine chenye chachu. Kamwe asinywe maji ya zabibu wala kula zabibu mbichi au kavu.

    5 " ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu hadi kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke. 6 Kwa kipindi chochote cha kujitenga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mnadhiri hatakaribia maiti.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    2 Law 10:9;Amu 13:4;Amo 2:12;Lk 1:15Nena na watu wa Israeli, uwaambie, Mwanamume au mwanamke atakapoweka nadhiri maalumu, nadhiri ya Mnadhiri,6:2 Au aliyewekwa wakfu. ili ajiweke wakfu kwa BWANA; 3 Lk 1:15atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yoyote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka. 5 Amu 13:5;1 Sam 1:11;Omb 4:7Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimguse kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa BWANA, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu. 6 Law 19:28;21:11;Yer 16:5,6;Eze 24:16-18;Mt 8:21Siku hizo zote ambazo alijiweka awe wa BWANA asikaribie maiti.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.