2 "Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Ikiwa mwanaume au mwanamke anataka kuweka nadhiri maalum, nadhiri ya kutengwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama Mnadhiri, 3 ni lazima ajitenge na mvinyo na kinywaji kingine chochote chenye chachu, na kamwe asinywe siki itokanayo na mvinyo au itokanayo na kinywaji kingine chenye chachu. Kamwe asinywe maji ya zabibu wala kula zabibu mbichi au kavu.
5 " ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu hadi kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke. 6 Kwa kipindi chochote cha kujitenga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mnadhiri hatakaribia maiti.