Misemo Ya Mfalme Lemueli
1 Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:
2 "Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu,
ee mwana wa nadhiri zangu,31:2 Au: Ewe uliye jibu la maombi yangu.
3 Usitumie nguvu zako kwa wanawake,
uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme.
4 "Ee Lemueli, haifai wafalme,
haifai wafalme kunywa mvinyo,
haifai watawala kutamani sana kileo,
8 "Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea,
kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa.
9 Sema na uamue kwa haki,
tetea haki za maskini na wahitaji."