Pular para o conteúdo
Publicidade

Mithali 31:1-4,8,9

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

1 Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:

2 "Sikiliza, ee mwanangu! Sikiliza, ee mwana wa tumbo langu!

Sikiliza, ee mwana wa nadhiri zangu!31:2 au Ewe uliye jibu la maombi yangu.

3 Usitumie nguvu zako kwa wanawake,

uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme.

4 "Ee Lemueli, haifai wafalme,

haifai wafalme kunywa mvinyo,

haifai watawala kutamani sana kileo,

8 "Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea,

kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa.

9 Sema na uamue kwa haki,

tetea haki za maskini na wahitaji."

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.

    2 Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu?

    Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?

    3 Kum 17:17;Neh 13:26;Mit 7:26;Hos 4:11Usiwape wanawake nguvu zako;

    Wala moyo wako usiwape wale wanaowaharibu wafalme.

    4 Mhu 10:17Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme;

    Wala haifai wakuu waseme, Kiko wapi kileo?

    8 Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu;

    Uwatetee watu wote walioachwa peke yao;

    9 Law 19:15;Kum 1:16;2 Sam 8:15;Isa 1:17,23;Zek 7:9;Yn 7:24;Ebr 1:9;Mit 21:13;Yer 22:16Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki;

    Uwapatie maskini na wahitaji haki yao.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:

    2 "Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu,

    ee mwana wa nadhiri zangu,31:2 Au: Ewe uliye jibu la maombi yangu.

    3 Usitumie nguvu zako kwa wanawake,

    uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme.

    4 "Ee Lemueli, haifai wafalme,

    haifai wafalme kunywa mvinyo,

    haifai watawala kutamani sana kileo,

    8 "Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea,

    kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa.

    9 Sema na uamue kwa haki,

    tetea haki za maskini na wahitaji."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.