Pular para o conteúdo
Publicidade

Warumi 11:32-36

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

32 Kwa maana Mungu amewafunga wanadamu wote kwenye kuasi ili apate kuwarehemu wote.

Wimbo Wa Shukrani

33 Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri

wa hekima na maarifa ya Mungu!

Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki,

na ambavyo njia zake zisivyotafutikana!

34 "Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Bwana?

Au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake?"

35 "Au ni nani aliyempa chochote

ili arudishiwe?"

36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake.

Utukufu ni wake milele! Amen.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    32 Kwa maana Mungu amewafunga wanadamu wote kwenye kuasi ili apate kuwarehemu wote.

    33 Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri

    wa hekima na maarifa ya Mungu!

    Tazama jinsi hukumu zake hazichunguziki,

    na ambavyo njia zake hazitafutiki!

    34 "Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Mwenyezi Mungu?

    Au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake?"

    35 "Au ni nani aliyempa chochote

    ili arudishiwe?"

    36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake,

    viko kwake na kwa ajili yake.

    Utukufu ni wake milele! Amen.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    32 Gal 3:22;1 Tim 2:4Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.

    33 Isa 55:8;45:15;Rum 9:23;10:12Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki! 34 Isa 40:13;Ayu 15:8;Yer 23:18;1 Kor 2:16Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? 35 Ayu 41:11Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? 36 1 Kor 8:6Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.