32 Kwa maana Mungu amewafunga wanadamu wote kwenye kuasi ili apate kuwarehemu wote.
Wimbo wa shukrani
33 Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri
wa hekima na maarifa ya Mungu!
Tazama jinsi hukumu zake hazichunguziki,
na ambavyo njia zake hazitafutiki!
34 "Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Mwenyezi Mungu?
Au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake?"
35 "Au ni nani aliyempa chochote
ili arudishiwe?"
36 Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake,
viko kwake na kwa ajili yake.
Utukufu ni wake milele! Amen.