Pular para o conteúdo
Publicidade

Warumi 15:8-13

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

8 Kwa maana nawaambia kwamba, Kristo amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonyesha kweli ya Mungu na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani, 9 pia ili watu wa Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake. Kama ilivyoandikwa:

"Kwa hiyo nitakutukuza katikati ya watu wa Mataifa;

nitaliimbia sifa jina lako."

10 Tena yasema,

"Enyi watu wa Mataifa, furahini

pamoja na watu wa Mungu."

11 Tena,

"Msifuni Bwana, ninyi watu wa Mataifa wote,

na kumwimbia sifa, enyi watu wote."

12 Tena Isaya anasema,

"Shina la Yese litachipuka,

yeye atakayeinuka ili kutawala juu ya mataifa.

Watu wa Mataifa watamtumaini."

13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    8 Kwa maana nawaambia kwamba Al-Masihi amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonesha kweli ya Mungu, na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani, 9 na pia ili watu wa Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake. Kama ilivyoandikwa:

    "Kwa hiyo nitakutukuza kati ya watu wa Mataifa;

    nitaliimbia sifa jina lako."

    10 Tena yasema,

    "Enyi watu wa Mataifa, furahini

    pamoja na watu wa Mungu."

    11 Tena,

    "Msifuni Mwenyezi Mungu, ninyi watu wa Mataifa wote,

    na kumwimbia sifa, enyi watu wote."

    12 Tena Isaya anasema,

    "Shina la Yese litachipuka,

    yeye atakayeinuka ili kuyatawala mataifa.

    Watu wa Mataifa watamtumaini."

    13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu wa Mungu.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    8 Mt 15:24;Mdo 3:25Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu; 9 2 Sam 22:50;Zab 18:49;Rum 11:30tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa,

    Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa,

    Nami nitaliimbia jina lako.

    10 Kum 32:43Na tena anena,

    Furahini, Mataifa, pamoja na watu wake.

    11 Zab 117:1Na tena,

    Enyi Mataifa yote, msifuni Bwana;

    Enyi watu wote, mhimidini.

    12 Isa 11:10;Ufu 5:5Na tena Isaya anena,

    Litakuwako shina la Yese,

    Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa;

    Ndiye Mataifa watakayemtumaini.

    13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.