8 Kwa maana nawaambia kwamba Al-Masihi amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonesha kweli ya Mungu, na kuthibitisha zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani, 9 na pia ili watu wa Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake. Kama ilivyoandikwa:
"Kwa hiyo nitakutukuza kati ya watu wa Mataifa;
nitaliimbia sifa jina lako."
10 Tena yasema,
"Enyi watu wa Mataifa, furahini
pamoja na watu wa Mungu."
11 Tena,
"Msifuni Mwenyezi Mungu, ninyi watu wa Mataifa wote,
na kumwimbia sifa, enyi watu wote."
12 Tena Isaya anasema,
"Shina la Yese litachipuka,
yeye atakayeinuka ili kuyatawala mataifa.
Watu wa Mataifa watamtumaini."
13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu wa Mungu.