10 "Piga kelele na ufurahie, ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni mwenu," asema Bwana. 11 "Mataifa mengi yataunganishwa na Bwana siku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwamba Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. 12 Bwana atairithi Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na atachagua tena Yerusalemu.
Publicidade
Publicidade