Pular para o conteúdo
Publicidade

Zekaria 6:1-8

Maono Ya Nane: Magari Manne Ya Vita

1 Nikatazama juu tena: nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba! 2 Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi, 3 la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. 4 Nikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, "Hawa ni nani bwana wangu?"

5 Malaika akanijibu, "Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. 6 Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini."

7 Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, "Nenda duniani kote!" Kwa hiyo wakaenda duniani kote.

8 Kisha akaniita, "Tazama, wale wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha Roho yangu katika nchi ya kaskazini."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.