Salamu
1 Paulo, niliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Al-Masihi Isa, na Sosthene ndugu yetu.
2 Kwa kundi la waumini wa Mungu walioko Korintho, kwa wale waliotakaswa katika Al-Masihi Isa na walioitwa kuwa watakatifu, pamoja na wale wote ambao kila mahali wanaliitia Jina la Al-Masihi Isa Bwana wetu, aliye Bwana wao na wetu pia.
3 Neema na amani zinazotoka kwa Mungu, Baba1:3 Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi. yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi ziwe nanyi.