24 naye baada ya kushukuru, akaumega, akasema, "Huu ndio mwili wangu, uliotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu." 25 Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu." 26 Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana Isa hadi ajapo.
Kushiriki Chakula cha Bwana Isa isivyostahili
27 Kwa hiyo, mtu yeyote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana Isa isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana Isa. 28 Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe.