Karama ya upendo
1 Hata kama nikisema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolia au toazi linalovuma. 2 Ningekuwa na karama ya unabii na kujua siri zote na maarifa yote, hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. 3 Nikitoa mali yote niliyo nayo, na nikijitolea mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.
13 Basi sasa, yanadumu mambo haya matatu: Imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu miongoni mwa haya matatu ni upendo.