24 Je, hamjui kwamba katika mashindano ya mbio wote wanaoshindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu apewaye tuzo? Kwa hiyo kimbieni katika mashindano ili mkapata tuzo.
25 Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji lisilodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji linalodumu milele. 26 Kwa hiyo mimi sikimbii kama mtu akimbiaye bila lengo, sipigani kama mtu anayepiga hewa. 27 La, bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha, ili nikiisha kuwahubiria wengine, nisije nikakataliwa.