11 Ndipo Nathani akamuuliza Bathsheba, mama yake Sulemani, "Je, hujasikia kwamba Adoniya mwana wa Hagithi, amekuwa mfalme pasipo bwana wetu Daudi kujua jambo hili? 12 Sasa basi, acha nikushauri jinsi utakavyookoa uhai wako mwenyewe na uhai wa mwanao Sulemani. 13 Ingia kwa Mfalme Daudi na umwambie, ‘Bwana wangu mfalme, je hukuniapia mimi mtumishi wako: "Hakika mwanao Sulemani atakuwa mfalme baada yangu na ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha ufalme"? Kwa nini basi Adoniya amekuwa mfalme?’