33 akawaambia: "Wachukueni watumishi wa bwana wenu pamoja nanyi na mkamkalishe mwanangu Sulemani juu ya nyumbu wangu mwenyewe, kisha mkamteremshe hadi Gihoni. 34 Huko kuhani Sadoki na nabii Nathani wampake mafuta awe mfalme juu ya Israeli. Pigeni tarumbeta na mpaze sauti, mkisema, ‘Mfalme Sulemani aishi maisha marefu!’ 35 Kisha mtapanda pamoja naye, atakuja na kuketi kwenye kiti changu cha ufalme na kutawala baada yangu. Nimemweka atawale juu ya Israeli na Yuda."
36 Benaya mwana wa Yehoyada akamjibu mfalme, "Amen! Mwenyezi Mungu, Mungu wa bwana wangu mfalme, na aamuru vivyo hivyo. 37 Kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa na bwana wangu mfalme, vivyo hivyo na awe na Sulemani kukifanya kiti chake cha utawala kuwa kikuu kuliko kile cha bwana wangu Mfalme Daudi!"
38 Hivyo kuhani Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, Wakerethi na Wapelethi wakaenda na kumpandisha Sulemani juu ya nyumbu wa Mfalme Daudi, nao wakamsindikiza hadi Gihoni.