Wakeze Sulemani
1 Mbali na binti Farao, Mfalme Sulemani aliwapenda wanawake wengi wa kigeni: Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti. 2 Walitoka katika mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliwaambia Waisraeli, "Msije mkaoana nao, kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu mgeukie miungu yao." Hata hivyo, Sulemani akakaza kuwapenda. 3 Alikuwa na wake mia saba, binti za uzao wa kifalme, na masuria mia tatu; nao wake zake wakampotosha. 4 Kadiri Sulemani alivyozidi kuzeeka, wake zake wakaugeuza moyo wake kuelekea miungu mingine, na moyo wake haukujitoa kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake.