9 Mwenyezi Mungu akamkasirikia Sulemani kwa sababu moyo wake uligeuka mbali na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, aliyekuwa amemtokea mara mbili. 10 Ingawa alikuwa amemkataza Sulemani kufuata miungu mingine, Sulemani hakutii amri ya Mwenyezi Mungu. 11 Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamwambia Sulemani, "Kwa kuwa huu ndio msimamo wako, na hukushika agano langu na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitakunyang’anya ufalme na kumpa mmoja wa walio chini yako. 12 Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi baba yako, sitafanya jambo hili wakati wa uhai wako. Nitaurarua kutoka mikononi mwa mwanao. 13 Lakini pia sitaurarua ufalme wote kutoka kwake, bali nitampa kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu na kwa ajili ya Yerusalemu, ambao nimeuchagua."
1 Wafalme 11:9-13
Em outras traduções
- SRUV Swahili Revised Union Version
9 Kum 7:3;Zab 90:7;1 Fal 3:5;9:2Basi BWANA akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha BWANA, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili, 10 1 Fal 6:12;9:6;2 Nya 7:17-22akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru BWANA. 11 1 Fal 12:15;2 Fal 17:15,21Kwa hiyo BWANA akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako. 12 Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako. 13 2 Sam 7:15;1 Nya 17:13,14;Zab 89:33;1 Fal 12:20;Kut 32:13;2 Fal 13:23;Kum 12:11;2 Fal 21:4;23:27;Zab 132:13,14;Isa 14:32;62:1,7Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
9 Bwana akamkasirikia Solomoni kwa sababu moyo wake uligeuka mbali na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye alikuwa amemtokea mara mbili. 10 Ingawa alikuwa amemkataza Solomoni kufuata miungu mingine, Solomoni hakutii amri ya Bwana. 11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Solomoni, "Kwa kuwa hii ndiyo hali yako na hukushika Agano langu na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme kutoka kwako na kumpa mmoja wa walio chini yako. 12 Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi baba yako, sitafanya jambo hili wakati wa uhai wako. Nitaurarua kutoka mikononi mwa mwanao. 13 Lakini pia sitaurarua ufalme wote kutoka kwake, bali nitampa kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu na kwa ajili ya Yerusalemu, ambao nimeuchagua."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.