33 Akapanga kuni, akamkata yule fahali vipande vipande na kuvipanga juu ya kuni. Kisha akawaambia, "Jazeni mapipa manne maji na kuyamwaga juu ya sadaka ya kuteketezwa na juu ya kuni."
34 Akawaambia, "Fanyeni hivyo tena." Nao wakafanya hivyo tena.
Akaagiza, "Fanyeni kwa mara ya tatu." Nao wakafanya hivyo kwa mara ya tatu. 35 Maji yakatiririka kuizunguka madhabahu na hata kujaza lile handaki.
36 Wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Ilya akasogea mbele na kuomba, akisema: "Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka na Israeli, ijulikane leo kwamba wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya mambo haya yote kama ulivyoagiza. 37 Unijibu, Ee Mwenyezi Mungu! Unijibu ili watu hawa wajue kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ndiwe Mungu, na kwamba unaigeuza mioyo yao ikurudie tena."
38 Kisha moto wa Mwenyezi Mungu ukashuka na kuiteketeza ile dhabihu, zile kuni, yale mawe, ule udongo, na pia kuramba yale maji yaliyokuwa ndani ya handaki.