Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Reis 18

41 Ilya akamwambia Ahabu, "Nenda, ukale na kunywa, kwa kuwa kuna sauti ya mvua kubwa." 42 Hivyo Ahabu akaondoka ili kula na kunywa. Lakini Ilya akapanda kileleni mwa Karmeli, akainama hadi chini, na kuweka kichwa chake katikati ya magoti.

43 Akamwambia mtumishi wake, "Nenda ukatazame kuelekea bahari." Akaenda na kutazama.

Akasema, "Hakuna kitu chochote huko."

Mara saba Ilya akasema, "Nenda tena."

44 Mara ya saba, mtumishi akaleta taarifa, "Wingu dogo kama mkono wa mwanadamu linainuka kutoka baharini."

Hivyo Ilya akasema, "Nenda ukamwambie Ahabu, Tandika gari lako la vita, ushuke kabla mvua haijakuzuia.’ "

45 Wakati ule ule anga likawa jeusi kwa mawingu, upepo ukainuka na mvua kubwa ikanyesha, naye Ahabu akaenda zake Yezreeli.

Veja também