Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Wafalme 19:11-13

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

11 Mwenyezi Mungu akasema, "Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu yu karibu kupita hapo."

Kisha upepo mzito na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la ardhi, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo kwenye lile tetemeko. 12 Baada ya tetemeko la ardhi moto ukaja, lakini Mwenyezi Mungu hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunong’ona. 13 Ilya alipoisikia, akafunika uso kwa vazi lake, akatoka na kusimama kwenye mlango wa pango.

Kisha ile sauti ikamwambia, "Ilya, unafanya nini hapa?"

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    11 Kut 24:12;Eze 1:4;37:7Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za BWANA. Na tazama, BWANA akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunjavunja miamba mbele za BWANA; lakini BWANA hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi; 12 Hes 14:18;Neh 9:17;Ayu 4:16;Zab 86:15;145:8;Yak 5:11na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu. 13 Kut 3:6;Isa 6:2Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya?

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    11 Bwana akasema, "Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za Bwana, kwa kuwa Bwana yu karibu kupita hapo."

    Kisha upepo mwingi na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za Bwana, lakini Bwana hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la nchi, lakini Bwana hakuwamo kwenye lile tetemeko. 12 Baada ya tetemeko la nchi ukaja moto, lakini Bwana hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunongʼona. 13 Eliya alipoisikia, akafunika uso kwa vazi lake, akatoka na kusimama kwenye mdomo wa pango.

    Kisha ile sauti ikamwambia, "Eliya, unafanya nini hapa?"

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.