4 lakini yeye mwenyewe akatembea mwendo wa kutwa nzima katika jangwa. Akafika kwenye mti wa mretemu, akakaa chini yake na kuomba ili afe. Akasema, "Yatosha sasa, Mwenyezi Mungu, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu." 5 Kisha akajinyoosha chini ya mti, akalala usingizi.
Mara malaika akamgusa na kumwambia, "Inuka ule." 6 Akatazama pande zote, na hapo karibu na kichwa chake palikuwa na mkate uliookwa kwenye makaa ya moto, na gudulia la maji. Akala na kunywa, kisha akajinyoosha tena.
7 Yule malaika wa Mwenyezi Mungu akaja tena mara ya pili, akamgusa na kumwambia, "Inuka ule, kwa kuwa bado una safari ndefu mbele yako." 8 Kwa hiyo akainuka, akala na kunywa. Akiwa ametiwa nguvu na kile chakula, akasafiri siku arobaini usiku na mchana hadi akafika Horebu, mlima wa Mungu. 9 Huko akaingia katika pango, akalala humo usiku ule.
Mwenyezi Mungu amtokea Ilya
Nalo neno la Mwenyezi Mungu likamjia, kusema, "Unafanya nini hapa, Ilya?"