5 Kisha akajinyoosha chini ya mti, akalala usingizi.
Mara malaika akamgusa na kumwambia, "Inuka ule." 6 Akatazama pande zote, na hapo karibu na kichwa chake palikuwa na mkate uliookwa kwenye makaa ya moto, na gudulia la maji. Akala na kunywa, kisha akajinyoosha tena.
7 Yule malaika wa Mwenyezi Mungu akaja tena mara ya pili, akamgusa na kumwambia, "Inuka ule, kwa kuwa bado una safari ndefu mbele yako." 8 Kwa hiyo akainuka, akala na kunywa. Akiwa ametiwa nguvu na kile chakula, akasafiri siku arobaini usiku na mchana hadi akafika Horebu, mlima wa Mungu.