11 Samweli akamuuliza, "Umefanya nini?"
Sauli akajibu, "Nilipoona kwamba watu wanatawanyika, na kwamba hukuja wakati uliopangwa na kwamba Wafilisti walikuwa wakikusanyika huko Mikmashi, 12 nikawaza, ‘Sasa Wafilisti watateremka dhidi yangu huko Gilgali nami sijaomba kibali kwa Mwenyezi Mungu.’ Hivyo nikalazimika kutoa sadaka ya kuteketezwa."