11 Hivyo akamuuliza Yese, "Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?"
Yese akajibu, "Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo."
Samweli akasema, "Tuma aitwe; hatutaketi hadi afike."
12 Basi akatuma aitwe, naye akaletwa. Aling’aa kwa afya, na mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.
Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, "Inuka na umpake mafuta; huyu ndiye."
13 Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumpaka mafuta mbele ya ndugu zake. Kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama.