Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 16:6,7,11-13

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

6 Walipofika, Samweli akamwona Eliabu, naye akafikiri, "Hakika mpakwa mafuta wa Mwenyezi Mungu anasimama hapa mbele za Mwenyezi Mungu."

7 Lakini Mwenyezi Mungu akamwambia Samweli, "Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. Mwenyezi Mungu hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini Mwenyezi Mungu hutazama moyoni."

11 Hivyo akamuuliza Yese, "Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?"

Yese akajibu, "Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo."

Samweli akasema, "Tuma aitwe; hatutaketi hadi afike."

12 Basi akatuma aitwe, naye akaletwa. Aling’aa kwa afya, na mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.

Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, "Inuka na umpake mafuta; huyu ndiye."

13 Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumpaka mafuta mbele ya ndugu zake. Kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    6 1 Fal 12:26Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi16:6 Au, mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10). wa BWANA yupo hapa mbele zake. 7 Zab 147:10;Isa 55:8;2 Kor 10:7;1 Fal 8:39;1 Nya 28:9;2 Nya 16:9;Zab 7:9;Yer 11:20;17:10;Mdo 1:24;Ufu 2:23Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.

    11 1 Sam 17:12;2 Sam 7:8;Zab 78:70Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hadi atakapokuja huku. 12 Wim 5:10;1 Sam 9:17Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. BWANA akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. 13 Zab 89:20;Hes 27:18;Amu 11:29;13:25;14:6Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu kuanzia siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    6 Walipofika, Samweli akamwona Eliabu, naye akafikiri, "Hakika mpakwa mafuta wa Bwana anasimama hapa mbele za Bwana."

    7 Lakini Bwana akamwambia Samweli, "Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. Bwana hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini Bwana hutazama moyoni."

    11 Hivyo akamuuliza Yese, "Je, hawa ndio wana pekee ulio nao?"

    Yese akajibu, "Bado yuko mdogo kuliko wote, lakini anachunga kondoo."

    Samweli akasema, "Tuma aitwe; hatutaketi mpaka afike."

    12 Basi akatuma aitwe naye akaletwa. Alikuwa mwekundu, mwenye sura nzuri na umbo la kupendeza.

    Ndipo Bwana akasema, "Inuka na umtie mafuta, huyu ndiye."

    13 Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea Roho wa Bwana akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.